Wednesday, February 10, 2016

LIVERPOOL YATOLEWA KOMBE LA FA NA WEST HAM




Ndoto za Liverpool kuwania kombe la FA zimefikia tamati baada ya kupokea kipigo kutoka kwa West Ham United katika mchezo wa pili wa marudiano uliochezwa katika wanja wa nyumbani wa West Ham, Queen Elizabeth Olympic Park.

Mchezo huo ulimalizika kwa West Ham kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja na ivyo kuitoa Liverpool kwa tofauti ya goli moja baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Anfield kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Magoli ya West Ham yalifungwa na Michail Antonio katika dakika ya 45 na baada ya muda mchache Liverpool ikasawazisha katika dakika ya 48 kupitia kwa Phillipe Coutinho na hadi dakika 90 zinamalizika walikuwa goli moja kwa moja.

West Ham ilipata goli la pili nala ushindi katika dakika ya 120 kupitia kwa Angelo Ogbonna na kuihakikishia West Ham kucheza hatua inayofata dhidi ya Blackburn ya Kombe la FA huku Liverpool ikitupwa nje ya mashindano hayo.

0 Responses to “ LIVERPOOL YATOLEWA KOMBE LA FA NA WEST HAM”

Post a Comment

More to Read