Wednesday, February 10, 2016
SERIKALI YASISITIZA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUINUA UCHUMI NCHINI.
Do you like this story?
Serikali
imesema dhamira yake ya kujenga uchumi wa viwanda nchini imejengwa kupitia
maeneo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti ijayo ya mwaka
wa fedha 2016/2017 kwa kutumia malighafi zipatikana nchini ikiwemo mzao ya
misitu, kilimo, uvuvi na madini ili kuwahudumia wananchi.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea
na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam.Dkt. Mpango aliyaeleza maeneo
hayo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti hiyo ni pamoja na
kuvirudisha viwanda vilivyobinafsishwa na kutafuta wabia ambao wanaweza
kufanyakazi iliyodhamiriwa.
Maeneo
mengine ni miradi mikubwa ya kielelezo ambalo wataalam wanalifanyiakazi ili
kuweza kupata matokeo makubwa, akitolea mfano Dkt. Mpango alisemas kuwa yapo
maeneo maalum ya kibiashara yakiwemo Bagamoyo,
Kigoma na Mtwara kutokana na
maliasili iliyopo hapo.
Zaidi
ya hayo, Dkt. Mpango aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda cha chuma kwa kutumia
malighafi inayozalishwa kwa kutumia chuma kutoka Liganga na Mchuchuma itakuwa
ni msingi wa viwanda mama ikizingatiwa “Hakuna ujenzi usiohitaji chuma”.
Katika
suala la ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, Dkt. Mpango alisema
kuwa mradi huo ni muhimu kwa lengo la kusukuma mbele sekta ya usafirishaji
ndani na nje ya nchi ikwemo nchi za Rwanda, Burundi Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) na mataifa mengine.
Mafanikio
ya ujenzi wa viwanda nchini yanawezekana kwa kwa kuwa Serikali imedhamiria
kushirikiana na serkta binafsi kwa kuwa maendeleo ya viwanda yanapaswa kuendana
na maendeleo ya watu kwa kuwapatia ajira, elimu inayoendana na mahitaji ya
viwanda ili maisha ya wananchi yawe bora zaidi.
Aidha,
ili kujenga uwezo wa kuwa na viwanda nchini, Serikali imejipanga kukusanya kodi
ambayo ndiyo msingi wa kuwa na uchumi imara utakaosaidia nchi kujiendesha
ambapo wafanyabiashara wote nchini wanapaswa kujisajili na kupewa namba ya
usajili (TIN) huduma ambayo inapatikana nchi nzima kupitia ofisi za Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA).
Katika
mkutana huo, Dkt. Mpango amewaasa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za
biashara yao ili kuwa na kumbukumbu ambazo zinatoa taarifa sahihi na kuhimiza
wafanyabiashara wenye mashine za kielekroniki (EFD) waendelee kuzitumia
wanapouza bidhaa zao na kuwaptia risiti wateja wao, kwa wale wasio na mashine
hizo,
Serikali
inaendelea kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kuwapatia mashine hizo.
Vile
vile, Dkt. Mpango ametoa namba za simu za ofisi za TRA kitengo cha Huduma na
Elimu kwa Mlipa Kodi ambapo wananchi wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na
Idara ya Mambo ya Ndani TRA juu ya maadili ya watumishi wa mamlaka hiyo nchi
nzima kwa namba 0689122515 na kutuma ujumbe mfupi kwa namba 0689122516.
Aidha,
Dkt. Mpango amewaonya wafanyabiashara ambao sio waaminifu waache
kufanyabiashara za magendo ambapo ameainisha baadhi ya maeneo yanayotumiwa ni
pamoja na mwambao wa bahari ya Hindi maeneo ya Mbweni, ziwa Victoria na ziwa
Tanganyika.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati na Sera TPSF Felix Mosha amesema kuwa
Sekta binafsi itaendelea kushirikiana na Serikali katika mpango wa kukuza
uchumi wa nchi na kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango kuwa
watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi na kuhamasisha wafanyabiashara wote nchini
wanakwenda pamoja na Sera ya “Hapa Kazi Tu”.
Imeandaliwa
na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YASISITIZA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUINUA UCHUMI NCHINI.”
Post a Comment