Tuesday, February 9, 2016

WACHEZAJI WA DR CONGO WATUZWA MAGARI YA KIFAHARI.


Rais Kabila amewapongeza wachezaji wa timu ya taifa

Kila mchezaji ametunukiwa gari la $60,000


Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa magari ya kifahari baada ya kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN).

Rais Joseph Kabila amemtunuku kila mchezaji gari gari la kifahari la thamani ya $60,000 (£40,000).
Wachezaji hao pia wamepewa nishani.
Chui hao wa Kinshasa walitwaa kombe kwa kulaza Mali 3-0 kwenye fainali na kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili.

anasema mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa kwamba atasafirishwa ng'ambo kwa matibabu.

0 Responses to “ WACHEZAJI WA DR CONGO WATUZWA MAGARI YA KIFAHARI.”

Post a Comment

More to Read