Friday, February 19, 2016

WAZIRI NAPE AMVUA MADARAKA MTENDAJI MKUU WA BARAZA LA MICHEZO (BMT)




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amemvua madaraka Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo (BMT), Henry Lihaya kwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kusaidia maendeleo ya michezo nchini.

Mhe. Nnauye alisema kuwa kama baraza hilo likitimiza wajibu wake linaweza kusaidia kukua kwa michezo lakini kasi ya michezo nchini inazidi kushuka na kutokana na wadau wa michezo kukosa pa kuelezea hisia zao hali inazidi mbaya zaidi.

“Nimefika ofisini hapa hata kibao kuonyesha kama hii ni ofisi ya Baraza la Michezo hakuna na hata hali ya utendaji wa kazi inaonyesha kuwa chini kama mkifanya kazi vizuri hata michezo itakua,” alisema Mhe. Nnauye.

Hivyo kutokana na sababu hiyo, Mhe. Nnauye amemvua madaraka Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo (BMT) na kumwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Elisante Oli Gabriel kumpangia kazi nyingine mtendaji mkuu huyo wizarani.

Pia kwa kanuni ya Baraza la Michezo, kifungu cha 5 (1) inamtaka Mwenyekiti wa Baraza kumchagua Mtendaji Mkuu na katika hilo Waziri Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa Baraza la Michezo, Dionis Malinzi kupendekeza majina ya watu ambao anataka wachukue nafasi ya utendaji mkuu kisha wizara itachagua Mtendaji Mkuu mpya.

0 Responses to “ WAZIRI NAPE AMVUA MADARAKA MTENDAJI MKUU WA BARAZA LA MICHEZO (BMT)”

Post a Comment

More to Read