Monday, March 14, 2016

CHANETA WAPIGA MSASA WALIMU 100 MBEYA.


Mwenyekiti wa Vijana  Mkoa wa Mbeya (Uvccm )Amani Kajuna ambae ndio Mgeni Rasmi akikabidhi Cheti kwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)



Washiriki wakiwa makini kumsikiliza Mgeni Rasmi..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Mwenyekiti wa Vijana  Mkoa wa Mbeya (Uvccm )Amani Kajuna ambae ndio Mgeni Rasmi akikabidhi Cheti kwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)



Mwenyekiti wa Vijana  Mkoa wa Mbeya (Uvccm )Amani Kajuna ambae ndio Mgeni Rasmi akikabidhi Cheti kwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)



Mwenyekiti wa Vijana  Mkoa wa Mbeya (Uvccm )Amani Kajuna ambae ndio Mgeni Rasmi akikabidhi Cheti kwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)




Ulifika muda wa keselebuka mara baada ya kupewa Vyeti na Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Vijana  Mkoa wa Mbeya (Uvccm )Amani Kajuna.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)



MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (Uv-CCM), Mkoa  wa Mbeya, Aman Kajuna, amewataka walimu waliofanikiwa kupata mafunzo ya taaluma ya michezo kuwa chachu ya kuibua vipaji na kustawisha michezo hapa nchni.

Kajuna alitoa wito huo juzi wakati akifunga mafunzo ya wiki mbili  kwa walimu wa mchezo wa mpira wa Pete kwa walimu zaidi ya 100 wa shule za msingi na sekondari, Mkoa wa Mbeya.

Amesema ili lengo la mafunzo hayo liendane na uhalisia, ni vizuri walimu hao waliopatiwa mafunzo kwa kushirikiana na Chama cha mchezo huo (Chaneta) kuhakikisha wanaibua vipaji kadili vinavyopatikana ili kustawisha mchezo huo.

Hata hivyo, aliwataka viongozi wanaoratibu walimu kushiriki mafunzo mbalimbali ya michezo kuteuwa walimu ambao kweli wanahusika na michezo, badala ya kupeleka walimu wasiokuwa na sifa ya kujihusisha na michezo.

Awali akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Ofisa michezo wa Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifamba, aliwataka walimu waliobahatika kupata mafunzo hayo kutumia fursa hiyo vizuri na kuwa chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika ufundishaji wa mchezo wa mpira wa netiboli kwa watoto.

‘’Napenda kuwakumbusha kuwa mmechaguliwa miongoni mwa walimu walio wengi kushiriki mafunzo haya hivyo, itumieni fursa mliyoipata vizuri na hata maporejea katika vituo vyenu vya kazi mkaache mtindo wa kufanya kazi kwa mazoea bali kujituma na kutanguliza uzalendo” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Cheneta Mkoa wa Mbeya, Shizya Mwakatundu alisema mafunzo hayo ya awali ya ualimu wa mchezo wa pete yatakuwa endelevu kwa lengo la kukuza mchezo huo.



0 Responses to “CHANETA WAPIGA MSASA WALIMU 100 MBEYA.”

Post a Comment

More to Read