Tuesday, March 8, 2016
CRDB MWANAFUNZI ALIYEONGOZA KIDATO CHA NNE AAHIDIWA AJIRA NA BENKI YA CRDB
Do you like this story?
Benki
ya CRDB imemfungulia Akaunti ya Scholarship
na kumwekea sh. Milioni 5 mwanafunzi aliyefanya
vizuri katika mtihani wa kumaliza kidato
cha nne mwaka 2015, Butogwa Shija na
kumwahidi ajira pindi amalizapo masomo.
Hafla
hiyo ilifanyika jana jijini Dar es
Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha
maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
leo, ambapo Butogwa alipewa zawadi ili
kuwahamasisha watoto wa kike kwamba wanaweza.
Pia
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilimuongezea
mwanafunzi huyo kiasi cha shilingi 500,000
lengo likiwa ni kuwahamasisha watoto wa
kike ili kuleta haki sawa kwa wote.
Naye
Butogwa aliahidi kutumia fursa hiyo vizuri
kwa kusoma kwa bidii bila kubweteka
na kuwataka wanafunzi wengine kuweka bidii
kwenye masomo yao.
Katika
hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Esther
Kitoka alisema wametoa sh. milioni 20
zitakazosaidia katika ujenzi wa mabweni kwa
watoto wa kike ili kuongeza kasi ya
ufaulu kwa wanafunzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ CRDB MWANAFUNZI ALIYEONGOZA KIDATO CHA NNE AAHIDIWA AJIRA NA BENKI YA CRDB”
Post a Comment