Tottenham imeshindwa kutumia uwanja wake wa nyumbani wa White Hart Line dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London, Arsenal baada ya kutoka sare ya goli mbili kwa mbili.

Magoli ya Tottenham katika mchezo huo yalfungwa na Toby Alderweireld dakika ya 60 na Harry Kane dk. 62 na magoli ya Arsenal yalifungwa na Aaron Ramsey dakika ya 39 na Alexis Sanchez katika dakika ya 76.

Baada ya matokeo hayo Tottenham imefikisha alama 55 ikiwa nafasi ya pili na Arsenal ikifikisha alama 52 ikiwa nafasi ya tatu, zote zikiwa zimeshacheza michezo 29.