Saturday, March 5, 2016
KASEJA NJE MBEYA CITY VS SIMBA KESHO
Do you like this story?
Kocha mkuu wa Mbeya City Fc , Kinnah Phiri
amesibitisha kuwa mlinda mlango mahiri wa kikosi chake Juma Kaseja
hatakuwa sehemu ya nyota watakaoiwakililisha City kwenye mchezo wa ligi
kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Simba Sports alub uliopangwa kuchezwa
jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
Muda mfupi uliopita kocha Phiri ameudokeza
mtandao huu kuwa ilikuwa waungane na kipa huyo leo asubuhi kwenye kambi ya muda
hapa Morogoro lakini imemlazimu kumuongezea muda zaidi wa kukaa karibu na
familia yake ili kushughulikia masuala kadhaa ya kifamilia aliyonayo hivi sasa.
“Wakati anaondoka Mbeya siku tano zilizopita tulikubaliana
kuwa ataungana nasi hapa siku ya leo, nimezungumza nae leo asubuhi kuna mambo
muhimu ya kifamilia amenieleza hivyo basi nimeamua kumuongezea siku
kadhaa za kubaki nyumbani kushughulikia yale yote yaliyopo kwenye
familia yake na imani yangu kuwa ataungana na kikosi mara tu tutakaporejea
mbeya kujiandaa na mchezo dhidi ya Stand United March 10.
Juma Kaseja aliondoka jijini Mbeya mara
baada ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Tanzania Prison
uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine kufuatia taarifa njema ya mkewe
kujifungua watoto mapacha.
Wachezaji wanzeke na uongozi wa City
kwa ujumla unampongeza Juma Kaseja na kumtakia kila la kheri
kwenye malezi ya watoto wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KASEJA NJE MBEYA CITY VS SIMBA KESHO”
Post a Comment