Saturday, March 12, 2016
KARATASI ZA KUPIGIA KURA ZAWASILI ZANZIBAR NA MAJINA YA WAGOMBEA WOTE PAMOJA WALITANGAZA KUSUSIA UCHAGUZI HUO
Do you like this story?
Picha za ujio wa Makatarsi na huyo anayeonekana hapo ni Mkurugenzi wa ZEC Salim Kassim Ali akitoa maelezo ya kuwasili kwake uwanja wa ndege Zanzibar. |
Karatasi za
kupigia kura kwa ajili ya marudio ya uchaguzi wa Zanzibar unaotarajiwa
kufanyika Machi 20, ziliwasili jana mchana visiwani hapa.
Karatasi hizo zilipokewa na watendaji mbalimbali wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), wakiongozwa na mkurugenzi wake, Salim Kassim katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Mkurugenzi huyo
aliwaeleza waandishi wa habari kuwa jumla ya karatasi 5,385 ndizo zilizowasili.
Kassim alisema
karatasi hizo zimechapishwa katika kiwanda cha Unprint cha Durban, Afrika
Kusini na ziliwasili hapo kwa ndege yenye Na EW-364TG ya nchi hiyo. Alisema
karatasi hizo pamoja na vifaa vingine vitasambazwa vituoni Machi 18, mwaka huu.
Kassim alisema
katika karatasi hizo za kupigia, yapo pia majina ya wagombea wote tisa wa vyama
vya upinzani waliokwishatangaza kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.
Miongoni mwa
wagombea hao ni Maalim Seif Sharif Hamad wa CUF, ambaye ametangaza kujitoa.
Uchaguzi huo wa
marudio, pia unaelezwa kugomewa na waangalizi wa kimataifa na hata wale wa
ndani.
Mbali na CUF
vyama ambavyo pia vimeeleza kutoshiriki uchaguzi huo ni Chaumma, Chama cha
Kijaamii (CCK), APPTMaendeleo, ACT-Wazalendo, Jahazi Asilia, Demokrasia Makini,
NRA na SAU.
Kassim
alipotakiwa kueleza sababu za ZEC kuchapisha karatasi za kura zenye wagombea
waliotangaza kususia uchaguzi huo wa marudio, alijibu kuwa yeye si msemaji.
Akizungumzia
gharama za uchaguzi huo wa marudio, mhasibu wa ZEC, Yussuf Ali Hassan alisema
utagharimu Sh4.5 bilioni tofauti na ule wa Oktoba 25, mwaka jana uliofutwa
ambao uligharimu kiasi ya Sh5.3 bilioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KARATASI ZA KUPIGIA KURA ZAWASILI ZANZIBAR NA MAJINA YA WAGOMBEA WOTE PAMOJA WALITANGAZA KUSUSIA UCHAGUZI HUO ”
Post a Comment