Wednesday, March 9, 2016
MCHEZAJI WA TANZANIA PRISONS ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA FEBRUARY
Do you like this story?
Mshambuliaji Mohamed Mkopi wa timu ya
Tanzania Prisons amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Februari kwa Ligi Kuu ya
Vodacom msimu huu wa 2015/2015.
Mkopi katika mwezi huo uliokuwa na raundi
nne, alicheza mechi zote nne za timu yake dhidi ya Mbeya City, Yanga, Mwadui na
Mgambo Shooting. Alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika mechi hizo
ambapo zote ilitoka sare, hivyo kupata jumla ya pointi nne.
Katika mechi hizo ambapo Tanzania Prisons
ilifunga mabao matatu, Mkopi alifunga bao moja na kusaidia kupatikana mabao mengine
mawili.
Mshambuliaji huyo ambaye mpaka sasa amefunga
mabao sita kwenye Ligi hiyo, aling’ara zaidi katika mechi mbili kati ya hizo
nne ambapo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Mkopi ambaye ni mshambuliaji wa kati
alichaguliwa mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya Mwadui iliyochezwa mkoani
Shinyanga, na ile dhidi ya Yanga iliyofanyika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora kwa
Februari, Mkopi atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na
wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Wachezaji bora wa miezi miwili iliyopita ni
kiungo Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba 2015), na beki Shomari Kapombe wa Azam
FC (Januari 2016).
Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MCHEZAJI WA TANZANIA PRISONS ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA FEBRUARY”
Post a Comment