Wednesday, March 9, 2016
MKWASA ATANGAZA 25 KUWAVAA CHAD
Do you like this story?
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premieum Lager, Charles Boniface Mkwasa jana ametangza kikosi cha
wa wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa
Afrika (AFCON) dhidi ya Chad, Machi 23, 2016 mjini Djamena.
Akiongea
na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho, Mkwasa amewaomba
wachezaji aliowaita katika kikosi hicho, kujiweka fit katika mazoezi
wanayoyafanya katika vilabu vyao, kwani hakutakua na muda wa kufanya mazoezi
kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.
“Ligi
Kuu ya Vodacom, michuano ya CAF (CL, CC) inachezwa wikiendi ya tarehe 18-20
Machi, hivyo wachezaji wote watakua na majukumu katiak timu zao, muda wa
kufanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mchezo huo hautakuwepo, ndio maana
nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda wenyewe kwa kuwa fit
wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo wa machi 23, 2016” alisema Mkwasa
Wachezaji
walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha
(Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi ni Juma Abdul, Haji
Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David
Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).
Viungo
Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi
Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa
(Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).
Washambuliaji
ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco
(Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na
Ibrahim Hajibu (Simba SC).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MKWASA ATANGAZA 25 KUWAVAA CHAD”
Post a Comment