Tuesday, March 8, 2016
NMB YATOA MAFUNZO YA KIJASIRIAMALI KWA WAFANYABIASHARA NCHINI
Do you like this story?
Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni Mh. Paul Makonda akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa hafla ya Business Club iliyofanyika Sinza jijini Dar es Salaam. |
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Vicky Bishubo akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni. |
Benki ya NMB PLC imetoa mafunzo ya
kijasiriamali kwa zaidi ya wafanyabiashara 300 jijini Dar es Salaaam. NMB ina
jumla ya vilabu vya biashara 34 nchi nzima vyenye wanachama zaidi ya 10,000.
NMB Business Clubs zina malengo ya kuwafikia jamii ya wafanyabiashara wadogo,
wa kati na wakubwa ambao wanajumuisha wafanyabiashara zaidi ya 50,000 ambao ni
wateja wa NMB nchi nzima.
Benki ya NMB PLC imekuwa kipaumbele
kuhamasisha wanafanyabiashara nchini kujikimu kimaisha kwa kufungua vituo vya
biashara nchini kimoja ambacho kipo kwenye wilaya ya Kinondoni- Sinza Business
Centre. Vituo hivi sio sehemu tuu ya kuchukulia mikopo bali pia ni sehemu ya
wafanyabiashara kupata ushauri kuhusu mikopo na biashara kutoka kwa wa
wataalamu wetu.
Kaimu Afisa wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB
PLC alisisitiza kwamba lengo kuu la vilabu hivi vya biashara
vimeundwa kuhakikisha wafanyabiashara nchini wanakuza mitaji yao, kuajiri
watanzania wengi zaidi na pia kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji
kodi.
Akiongea na wafanyabiashara nchini Mkuu wa
Wilaya wa Kinondoni Paul Makonda ameipongeza benki ya NMB kwa kuonyesha shauku
ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi kupitia vilabu vya biashara ambavyo vinawapa
wananachi elimu ya kijasiriamali na hivyo kupiga hatua ya kuiuchumi kimaisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NMB YATOA MAFUNZO YA KIJASIRIAMALI KWA WAFANYABIASHARA NCHINI”
Post a Comment