Tuesday, March 8, 2016
Paul Makonda Aibuka na Ubunifu Mwingine....Asema Anampango wa Kuanzisha Mtaa Maalumu Kinondoni Kwa Ajili ya Biashara ya Pombe ( Bar)
Do you like this story?
Siku tatu baada
ya kutoka India alikokwenda kwa ajili ya kupata matibabu, Katibu Mkuu wa Chama
Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana alilazwa katika hospitali ya
Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu
Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassoro Mazrui amesema kuwa chanzo cha Maalim Seif
kulazwa katika hospitali hiyo jana asubuhi ni uchovu wa safari yake ya India
ambayo alienda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.
Mazrui
alikanusha taarifa zilizokuwa zinaenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa
kiongozi huyo wa CUF alilazwa kutokana na matatizo ya moyo. Alisema kuwa hakuna
kumbukumbu yoyote ya ripoti ya daktari inayoonesha kuwa Maalim Seif ana tatizo
la moyo.
Naibu Katibu
Mkuu huyo wa CUF alisema kuwa kiongozi huyo anaendelea vizuri kiafya na kwamba
hayuko katika hali mahututi kama ilivyokuwa ikielezwa.
“Anakula na
kufanya kila kitu mwenyewe na hata jioni hii nimeongea naye, anakula kila kitu,
hivyo Watanzania wasiwe na wasiwasi juu ya afya ya Maalim Seif,” alisema
Mazrui.
Viongozi
mbalimbali wa vyama vya siasa waliwasili katika hospitali hiyo kumjulia hali
akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Paul Makonda Aibuka na Ubunifu Mwingine....Asema Anampango wa Kuanzisha Mtaa Maalumu Kinondoni Kwa Ajili ya Biashara ya Pombe ( Bar) ”
Post a Comment