Wednesday, March 9, 2016

RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG AWASILI TANZANIA



Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakiwapungia mkono viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakiteta jambo wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 08 Maachi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akiangalia vikundi vya ngoma vikivyotumbuiza uwanjani mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa

0 Responses to “RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG AWASILI TANZANIA”

Post a Comment

More to Read