Sunday, March 6, 2016

RONALDO APIGA NNE, MADRID IKISHINDA GOLI 7 - 1 DHIDI YA CELTA VIGO





Staa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameisaidia timu yake ya Real Madrid kuibuka na ushindi mnono wa goli saba kwa moja walipokuwa wakipambana na Celta Vigo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania.

Ronaldo alifunga magoli hayo katika dakika ya 50, 58, 65 na 76 na hivyo kufikisha hat trick ya 36 katika historia yake ya maisha ya soka.

Magoli mengine ya Real Madrid yalifunga na Pepe dk. 41, James Rodriguez dk.78 na Gareth Bale dakika ya 81 na goli pekee la Celta Vigo likifungwa na Iago Aspas dk.62.

Baada ya ushindi huo Madrid imefikisha alama 60 ikiwa nyuma kwa nafasi moja na Atletico Madrid iliyo katika nafasi ya pili.

0 Responses to “RONALDO APIGA NNE, MADRID IKISHINDA GOLI 7 - 1 DHIDI YA CELTA VIGO”

Post a Comment

More to Read