Sunday, March 6, 2016
SIKIA HII>>>> SAA ZINAZOWEZA KUTUMIWA KUIBA MITIHANI (CHABO).
Do you like this story?
Saa za kisasa
ambazo zimetengenezwa mahususi kutumiwa kudanganya wakati wa mtihani zimekuwa zikiwakosesha
usingizi walimu na wasimamizi wa mitihani.
Saa hizo zina
uwezo wa kuweka akiba data na maelezo ambayo yanaweza kusomeka mtu anapofanya
mtihani.
Aidha, zina
kitufe cha dharura ambacho kinaweza kubadili uso wa saa hizo haraka sana na
badala ya kuonesha habari ziwe zinaonesha uso wa kawaida wa saa.
Saa hizo
zinatangazwa katika soko la kuuza bidhaa mtandaoni la Amazon.
Mojawapo ya
aina ya saa hizo ina uwezo wa kuweka akiba data ya 4GB. Nyingine, ambayo
itaanza kuuzwa baadaye mwaka huu, itakuwa na uwezo wa 8GB na inaweza kuhifadhi
hata video.
Baadhi ya saa
hizo, zina kifaa kidogo sana cha kusikizia ambacho hakitumii nyaya, jambo
linalowezesha mtu kusikiliza kilichohifadhiwa kwenye saa hiyo bila kuonekana.
Tangazo moja
katika mtandao wa Amazon linasema mtu anaweza kununua saa ya aina hiyo kwa $61
(£43).
Kuna pia
matangazo ya saa hizo eBay.
Naibu mwalimu
mkuu wa shule moja kutoka Bath, Uingereza anasema saa hizo zinaweza
zikawashawishi wanafunzi kuhadaa katika mtihani.
Bw Joe Sidders
wa shule ya Monkton Combe Senior School amesema ingawa saa hizo zinaweza
kudhibitiwa kwa kutumia sheria zinazoharamisha simu na kompyuta kutoka vyumba
vya mitihani, ni changamoto kubwa sana kwa watu wanaosimamia mitihani.
Amesema uuzaji
wa saa hizo unafaa kudhibitiwa.
Kuna pia
“kalamu za kuiba mtihani” ambazo zinaweza kuhifadhi habari na maelezo.
Ongezeko la
matumizi ya saa kuiba yamefanya baadhi ya mashirika kupiga marufuku saa katika
vyumba vya mitihani Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIKIA HII>>>> SAA ZINAZOWEZA KUTUMIWA KUIBA MITIHANI (CHABO). ”
Post a Comment