Thursday, May 5, 2016

- WANANCHI TANDALA MAKETE WAZUNGUMZIA KAMATAKAMATA YA WANAOLEWA MUDA WA KAZI




Siku chache baada ya sheria ya kukamata watu wanao kunywa pombe saa za kazi kuanza kutekelezwa ktk kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe baadhi wananchi wa kijiji CHA TANDALA wametoa maoni yao.

Wananchi hao wametoa maoni yao walipokuwa wakizungumza na kituo cha Green fm kwa nyakati tofauti ambapo wamesema sheria iongozewe nguvu zaidi katika utoaji wa adhabu na wengine wakisema adhabu ni kubwa hivyo wapungunzwe.

Katika hatua nyingine wananchi hao wamesema utekelezwaji wa sheria hiyo ya kutokunywa pombe muda wa kazi ilenge kwa watu wote bila ya kuchagua sehemu ya kukamata.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Tandala Bi Karmela Malley amekanusha tuhuma za kwamba wanabagua kukamata watu wanao kunywa pombe muda wa kazi na kubainisha kuwa wao wanafuata sheria.

Bi Malley amesema saa yoyote na siku yoyote oparesheni inafanyika na kuwataka wananchi kuondoa wasiwasi na wafuate sheria.

Na Asukile Mwalwembe

 

0 Responses to “ - WANANCHI TANDALA MAKETE WAZUNGUMZIA KAMATAKAMATA YA WANAOLEWA MUDA WA KAZI”

Post a Comment

More to Read