Thursday, May 5, 2016
WABUNGE WAGOMEA UTARATIBU WA KUJISAJILI MARA MBILI....WADAI WAO NI WATU WAZIMA NASIO WANAFUNZI
Do you like this story?
Wabunge
wameitaka Ofisi ya Bunge iwaondolee mara moja utaratibu wa kusaini kwa kutumia
vidole mara mbili kwa siku kwa kuwa wao si wanafunzi.
Hoja hiyo
iliwasilishwa kwa njia ya mwongozo na kuungwa mkono na wabunge wote isipokuwa
mawaziri na Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) mjini Dodoma jana.
Katika
Mwongozo wake, mbunge huyo alisema kitendo cha kutakiwa kusaini mara mbili kwa
siku ni kero kwa wabunge na uonevu kwa kuwa hata Bunge limekuwa likitumia muda
wa mapumziko wa wabunge kwa kazi za Bunge.
“Mheshimiwa
Naibu Spika wewe mwenyewe muda mfupi umetangaza matangazo mbalimbali yanayotaka
baadhi ya wajumbe wa kamati wakutane baada ya saa saba mchana, tunafanya kazi
nje ya mapumziko yetu, haya haina tatizo... “...tatizo langu ni kitendo cha
wabunge kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, wakati mwingine
tunatoka hapa saa saba, wabunge tunashughulikia mambo mpaka saa 12, mbunge
anatumia muda wake wa mapumziko na ule wa kuhudhuria kikao cha jioni,” alisema Haji.
Alisema
inasikitisha kuona mbunge anatolewa kwenye kazi za kujenga taifa ili aje tu
asaini kwa kidole tena mara ya pili.
Alisema
jambo hilo linawatatiza wabunge kwa kuwa wanajiona kama wanachukuliwa kama
wanafunzi kwa kufuatiliwa kwani hata kwenye benki wafanyakazi hawasaini na
kufuatiliwa kama ilivyo kwa wabunge hao.
Alifafanua
kuwa kabla ya kuomba Mwongozo huo, alifanya utafiti kwenye benki mbalimbali
ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambao nao wana utaratibu kama huo wa Bunge
lakini hakuna mahali wanapotakiwa kusaini kwa vidole mara mbili.
“Kutokana
na uzito wa jambo hili naomba kutoa hoja wabunge mniunge mkono mpango huu
ukome,” alisema na wabunge takribani wote
walisimama ishara ya kumuunga mkono na kumpigia makofi na vigelegele.
Kwa upande
wake, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema kutokana na namna wabunge hao
walivyopokea suala hilo, pamoja na kwamba kikanuni jambo hilo halikutakiwa
kuombewa mwongozo bado litaangaliwa.
“Hata
hivyo, nifafanue kuwa kusaini mara mbili lengo lake si kuwafanya wabunge
wanafunzi, ila lengo ni kutaka kujua nani wapo humu ndani (bungeni),” alisema Dk Ackson.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WABUNGE WAGOMEA UTARATIBU WA KUJISAJILI MARA MBILI....WADAI WAO NI WATU WAZIMA NASIO WANAFUNZI”
Post a Comment