Wednesday, August 24, 2016

KOFIA YA MZEE AKILIMALI YARUDISHWA



Kofia ya Katibu wa Baraza la wazee katika klabu ya Yanga Mzee Ibrahim Akilimali hatimaye imepatikana baada ya alieichukua kuirudisha polisi.

Mzee Akilimali ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kipindi cha hivi karibuni baada ya yeye kupinga wazo la Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kutaka kuichukua timu ya Yanga kwa mkopo, alipoteza kofia yake wakati alipomtembelea mzee mwenzake Hashim Mhika, Mtoni. Kofia yake ilipotea wakati alipomfuata mzee mwenzake katika mkeka na kuiacha kofia yake chini na aliporudi watoto wa mjini tayari walikuwa wameshaiichukua.

 




Alipoulizwa kuhusiana na kupotea kwa kofia yake Mzee Akilimali alisema kuwa kwa vyovyote vile lazima alieichukua atairudisha na kweli hatimaye alieichukua ameirudisha na tayari mzee Akilimali amethibitisha kuwa kofia yake imepatikana.
 
Mzee Akilimali alijijengea umaarufu kutokana na staili yake aliyoitumia wakati baadhi ya wazee walipotofautiana na uongozi wa Lloyd Nchunga. Mzee Akilimali aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelezea machungu yake kisha akasema wao kama wazee wanavua kofia (kasha wakazivua na kuziweka mezani). Kilichofuata ni Yanga kufungwa tano na Simba, matokeo yaliyoambatana na Nchunga kubwaga manyanga.

 Source #TanzaniaDaima

0 Responses to “KOFIA YA MZEE AKILIMALI YARUDISHWA ”

Post a Comment

More to Read