Tuesday, August 23, 2016

USAIN BOLT ATEMBEA NA MJANE WA MUUZA UNGA



Mwanariadha maarufu Duniani Usain Bolt (30) ambaye ameweka historia katika mashindano ya riadha kwa kushinda medali za zahabu katika mashindano ya mita 100, 200 na 4 x 100m ameingia katika kasha kubwa baada ya picha zake kuvuja akiwa na mwanafunzi wa miaka 20, Lady Duarte ambaye pia aliwahi kuwa ni mpenzi wa muuza madawa wa nchini Brazil  Dina Terror.




Bolt ambaye amekuwa akionesha maisha ya Furaha muda wote na mpenzi wake wa siku nyingi (miaka 2) Kasi Bennett, ameishangaza dunia baada ya picha hizo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Pamoja na kumsapoti mchumba wake wa siku nyingi Kasi Bennett alifuta picha zote za Bolt kwenye  akaunti yake ya Twitter masaa machache baada ya kusambaa kwa picha hizo na baadae kuifuta kabisa akaunti yake ya Twitter.





Picha hizi zilipigwa na Lady Duarte siku ya kuzaliwa kwa Bolt Jumapili iliyopita tarehe 21 ambapo Bolt alkuwa akitimiza miaka 30.

0 Responses to “USAIN BOLT ATEMBEA NA MJANE WA MUUZA UNGA ”

Post a Comment

More to Read