Tuesday, August 23, 2016
WEZI FEDHA ZA TASAF KIKAANGONI
Do you like this story?
SERIKALI
imetoa siku 30 kukamatwa kwa watumishi waliosababisha matumizi mabaya ya fedha
za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) III, kwa kuingiza majina ya
watu masikini wasiostahili ili kujipatia fedha za mradi huo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George
Simbachawene akizungumza na baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi,
jana alisema ni lazima watumishi wa umma waliohusika katika kuisababishia
hasara Serikali wawajibishwe.
Februari
mwaka huu, TASAF ilitekeleza maagizo ya Serikali na kufanya uhakiki wa kaya
masikini ziliopo kwenye mpango wa kupata fedha na kuziondoa zile zilizokosa
sifa na kuziondoa kaya 32,456.
“Katika
msako huo tulibaini, waliokufa ni 7,819, viongozi waliojipachika 2,999,
waliohama sehemu ambapo mpango haujaanza 3,948, wasiojitokeza au wasiofahamika
9,342 na wasiokuwa na sifa 8, 348,”
alisema Simbachawene.
Aidha
alisema kuwa, zoezi hilo ni endelevu na kwamba utaratibu wa kutoa taarifa za
walengwa waliofariki au kuhama unapaswa kufanyika ili fedha za serikali
zisitumike ovyo nje ya malengo yaliyokusudiwa.
Simbachawene
alisema, kuingizwa kaya zisizo na sifa katika mpango huo na kuachwa kwa kaya
ambazo ni maskini zaidi, kumetokana na baadhi ya watumishi wasio waadilifu
ambao pia wamekuwa wakipunguza malipo ya walengwa.
Watu
6.5 milioni, katika kaya maskini na zinazoishi katika mazingira hatarishi
wanatarajiwa kunufaika na mradi wa fedha za TASAF katika awamu ya sasa.
Hata
hivyo, Simbachawene aliwashauri wakurugenzi wa halmashauri zote nchini pamoja
na wakuu wa wilaya, kutoogopa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria,
kanuni na taratibu zilizopo kwani suala hilo litaepusha hasara na mianya ya
wizi.
Mhandisi
Evarist Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alimuahidi waziri Simbacahwene kuwa,
hawatofumbia macho ubadhirifu katika halmashauri na kusema watazishauri,
kuzikumbusha na hata kuingilia kati pale mambo yanapoenda ndivyo sivyo katika
halmashauri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ WEZI FEDHA ZA TASAF KIKAANGONI”
Post a Comment