Monday, August 22, 2016
MSOMALI FEYISA LILESA ASHINDA MEDALI YA SILVER LAKINI ANAOGOPA KURUDI KWAO
Do you like this story?
Mwanariadha
kutoka Taifa la Ethiopia Feyisa Lilesa amefanikiwa kushinda medali ya Shaba
katika mbio za marathon kwenye michuano ya Olimpiki Rio Brazili
lakini anaogopa kurudi nchini kwao kwa hofu ya kuuliwa au kufungwa jela.
Hi imekuja
baada ya Lilesa kuonesha alama ya msalaba kwa kutumia mikono yake wakati
akimalizia kuvuka mstari wa mwisho, ishara hii hutumika na waandamanaji
wanaopinga serikali iliopo madarakani nchini Ethiopia.
Akiongea na
vyombo vya habari baada ya tukio hili alisema “nilionesha vile katika kusapoti
familia yangu na ndugu zangu ambao wamefungwa jela”
“Kama nikiamua
kurudi nyumbani wataniua, na kama sio kuniua basi watanifunga au kunizuia pindi
nitakapotua uwanja wa ndege, hivyo nimeamua kwenda kwenye nchi nyingine kwa
sasa” aliongeza Lilesa.
Katika maelezo
yake aliendelea kusisistiza kuwa serikali iliyopo madarakani ni serikali mbaya
na onevu ambayo pindi mataifa ya Marekani, Uingereza na Ufaranza wanapowapa
sapoti basi wao hutumia fedha hizo kwenye kununulia silaha ambazo huzitumia
kuulia watu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)



0 Responses to “MSOMALI FEYISA LILESA ASHINDA MEDALI YA SILVER LAKINI ANAOGOPA KURUDI KWAO ”
Post a Comment