Sunday, August 21, 2016
UCHAGUZI CONGO WAHAIRISHA, KABILA KUONGOZA HADI 2017
Do you like this story?
Tume ya
Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetangaza kuahirishwa uchaguzi
wa rais nchini humo hadi mwezi Julai 2017.
Habari
hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kongo, Corneille Nangaa
na kuongeza kuwa, shughuli ya uandikishaji majina ya wapiga kura iliyoanza
mwezi Machi mwaka huu, itachukua muda wa miezi 16 hadi kukamilika.
Awali
mahakama ya juu ya nchi hiyo ilitangaza kuwa iwapo serikali ya Rais Joseph
Kabila haitaweza kuanda uchaguzi wa rais katika wakati ulioainishwa basi
kiongozi huyo anaweza kubakia madarakani hadi wakati wa kufanyika uchaguzi
mkuu.
Kabila
alishika hatamu za kuiongoza Congo mwaka 2001 baada ya mauaji ya baba yake,
Laurent Kabila, na kisha akashinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka 2006.
Kwa
mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rais Joseph Kabila
haruhusiwi kugombea tena kiti hicho baada ya kuongoza katika vipindi viwili vya
Miaka 5 mfululizo.
Na Regina
Mkonde
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ UCHAGUZI CONGO WAHAIRISHA, KABILA KUONGOZA HADI 2017”
Post a Comment