Sunday, August 21, 2016
SERENGETI BOYS YAWAJAZA FURAHA WATANZANIA, YAWAFUMUA 'WASAUZI' CHAMAZI.
Do you like this story?
Timu
ya taifa ya vijana chini miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imepata ushindi wa magoli
2-0 dhidi ya timu ya vijana ya Afrika Kusuni katika mchezo wa marudiano
uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex kuwania kufuzu fainali za matifa ya
Afrika kwa vijana wa umri huo mashindano yanayotarajiwa kufanyika Madagascar.
Magoli
ya Serengeti Boys yamefungwa na kipindi Mohamed Abdala aliyefunga dakika ya 34
kipindi cha kwanza wakati bao la pili likifungwa dakika za lala salama na
Muhsin Makame.
Serengeti
Boys imeitupa nje timu ya taifa ya Afrika Kusini kwa jumla ya magoli 3-1 hiyo
ni baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa awali
uliopigwa Afrika Kusini.
Matokeo
hayo yanaifanya Serengeti Boys isonge mbele, itakutana na Namibia au Congo
Brazzaville katika raundi inayofuata na endapo itafanikiwa kufuzu basi itakata
tiketi ya kushiki katika fainali za mataifa ya Afrika.
Ally
Ng’anzi wa Serengeti Boys alioneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo baada ya
kuoneshwa kadi mbili za njano hivyo ataukosa mchezo mmoja ujao wa timu yake.
September
mwaka huu Serengeti itakuwa mwenyeji wa Namibia au Congo Brazzaville huku
mchezo wa marudiano ukitarajiwa kuwa kupigwa mwezi October.
-
See more at: http://www.barakampenja.com/2016/08/serengeti-boys-yawajaza-furaha.html#sthash.AbaiuJUr.dpuf
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)




0 Responses to “SERENGETI BOYS YAWAJAZA FURAHA WATANZANIA, YAWAFUMUA 'WASAUZI' CHAMAZI.”
Post a Comment