Monday, August 29, 2016

YAFAHAMU MATUKIO MANNE MAKUBWA SEPTEMBER MOSI


Septemba mosi mwaka huu inatarajiwa kuwa siku ya kipekee kutokana na nchi yetu kuwa na matukio makubwa manne ya kihistoria ambayo yamekuwa yakisubiriwa kwa hamu na watanzania wengi nchini.

Matukio hayo ni :-

1. Tukio la kupatwa kwa jua tukio hili ni la kihistoria likijirudia baada ya miaka 36 iliyopita, Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zitaweza kushuhudia tukio hillo vizuri katika mji wa Lujewa Wilayani Mbarare mkoani Mbeya na maeneo mengine kama Katavi,Ruvuma na Masasi.

2. Maadhimisho ya Miaka 52 ya Jeshi la Wananchi (JWTZ)
Jeshi la wananchi linatarajiwa kuadhimisha miaka 52 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 kwa kufanya zoezi la kufanya  usafi katika maeneo tofauti.
Mbali na usafi madaktari wa JWTZ watatoa huduma tiba bure kama upimaji wa virusi vya Ukimwi, Kisukari na shinikizo la damu na kushiriki katika michezo mbalimbali na Taasisi nyingine.

3. Maandamano ya  Chadema (UKUTA)
Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kufanya maandamano nchi nzima kupinga kauli ya Mh Rais Dkt. John Magufuli ya kufungia mikutano yote ya vyama vya siasa nchini

Maandamano hayo yanaleta sura nyingine kwani jeshi la Polisi Nchini limejiandaa kukabiliana na kundi lolote litakalokuwa likifanya maandamano siku hiyo kwani watakua wamekiuka kauli ya Mh Rais, tangu chama cha CHADEMA kutangaza siku hiyo jeshi laPolisi limeonekana katika mikoa mbalimbali kufanya mazoezi ambayo ni sehemu ya kawaida ya jeshi hilo huku baadhi ya watu wakiielezea kuwa ni sehemu ya kujiandaa na maandamano hayo yaliyopewa jina maarufu UKUTA

4. Waziri Mkuu kuhamia rasmi Dodoma
Septemba mosi ni siku ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuhamishia ofisi yake Rasmi Mkoani Dodoma kwa kutekeleza agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli la kutaka Serikali ihamie katika mji ambao ndio Makao Makuu ya Nchi (Dodoma)
Majaliwa atakuwa ndio Kiongozi wa kwanza kuhamia Dodoma huku  baadhi ya mawaziri wengine  kuahidi kutekeleza agizo hilo mwezi Septemba mwaka huu.
 


0 Responses to “YAFAHAMU MATUKIO MANNE MAKUBWA SEPTEMBER MOSI”

Post a Comment

More to Read