Monday, August 29, 2016
BARAZA KUU LA CUF LAMVUA UANACHAMA PROF. LIPUMBA NA WENZAKE
Do you like this story?
Taarifa zilizotufikia hivi punde
zinaeleza kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim
Lipumba, Mbunge wa Kaliuwa, Mbunge wa Mtwara Mjini, Mkurugenzi wa Habari na
wafoasi 10 wengine wamevuliwa rasmi uanachama CUF.
Uamuzi huo unaelezwa kuwa ni uamuzi
wa Baraza kuu lililoketi huko visiwani Zanzibar.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari Abdul
Kambaya ameyaandika haya,
Nimekuwa napigiwa simu nyingi toka
kwa Wanachama wenzangu na Waandishi wa habari kuhusu Taarifa zilizozagaa kwenye
Mitandao. Majibu yangu ya awali Kuhusu Taarifa hizo ni
1) Moja Baraza Kuu lina Mamlaka ya
kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na kwa kwa kufuata Katiba jinsi inavyoeleza
kwenye hizo taratibu za kuchukua hatua za Kinidhamu.
2) Mimi na wenzangu tunaotajwa kwenye
kadhia hiyo ikiwa ni Pamoja na Wabunge wa Mtwara Mjini (Maftaha Nachuma) na
Magdalena Sakaya Mbunge wa Jimbo la Kaliua na Diwani wa Kata ya Misima Wilayani
Handeni,pamoja na wale ambao sikuwataja hatukuwepo wakati hukumu hiyo inatolewa
na Baraza Kuu lilofanyika jana Mjini Unguja katika Visiwa vya Zanzibar.
3) Baada ya kuahirishwa kwa Mkutano
Mkuu uliofanyika pale Ubungo Plaza Tarehe 21 /08 /2016 kutokana na Wajumbe 324
kutoridhishwa na ukiukwaji wa Katiba ya Chama chetu ikiwa ni pamoja na kuingizwa
kwa Wajumbe wasio halali kwenye Mkutano Mkuu, mimi ni miongoni mwa Wajumbe
tuliojiorodhesha na kuandika barua ya Malalamiko na kupeleka Ofisi ya Msajili
wa Vyama.
Kutokana na Mambo hayo Matatu,
nawaomba Wanacuf msifadhahike na wala msihuzunike waliotufukuza kabla hata ya
kutoa majibu ya hoja zetu tulizowasilisha kwa Msajili, bila shaka hawana Majibu
ya sahihi ya hoja zetu. Na jambo hili sio geni kwa hapa Duaniani, Firaun
aliposhindwa kuthibitisha kua yeye ndie Mungu, alitumia Jeshi lake (Baraza Kuu)
kutaka kumuangamiza Mussa na Wafuasi wake waliokua wanaamini katika Haki na
Mungu wa kweli.
Kilichoendelea Zanzibar ni Mfano wa
Firaun na Jeshi lake dhidi ya Mussa na Wafuasi wake.
Kauli yangu ya Mwisho ni kwamba
hatoki mtu kwenye Cuf hii kwakua sio ya Mtu bali ni ya watu, sijambo jema
kujifananisha na Firaun, jibu hoja usitumie Jeshi kujibu hoja. Hakuna kukataa
Tamaa wala kukimbia CUF. Harakati za kutafuta
Fahari News inaendelea kufuatilia kwa
kina kuhusiana na habari hii ili kuweza kujua undani wake kwa kina na
kukuhabarisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “BARAZA KUU LA CUF LAMVUA UANACHAMA PROF. LIPUMBA NA WENZAKE”
Post a Comment