Monday, August 29, 2016

KONDOM YA ZANA RASMI KUZINDULIWA KESHO MKOANI MBEYA


Kaimu Mkurugenzi wa Elimu, Habari na mawasiliano, kutoka Wizara ya Afya kitengo cha Kudhibiti Ukimwi (TAC AIDS)Edah Charles akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).




Baadhi ya Waandishi na waelimishaji wakisikiliza elimu kutoka kwa watoa Maada kutoka Wizara ya Afya.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kondomu mpya inayotolewa na Serikali aina ya Zana utakaofanyika kesho katika ukumbi wa Mkapa Sokomatola jijini Mbeya.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari katika kikao kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa, Kaimu Mkurugenzi wa Elimu, Habari na mawasiliano, kutoka Wizara ya Afya kitengo cha Kudhibiti Ukimwi (TAC AIDS)Edah Charles alisema Kondom hiyo aina ya ZANA itatolewa bure kwa wananchi.

Alisema lengo la uzinduzi wa Kondom hizo ni kuhamasisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya Kondom ambazo zitatolewa bure kupitia vituo maalum vitakavyowekwa na kuandaliwa ili kila mtumiaji aweze kupata kirahisi.

Aliongeza kuwa lengo ka kuzindulia Mbeya ni kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha maambukizi hivyo kutoa fursa kwa wananchi kuweza kufanikisha kuhakikisha Nchi inafanikiwa kuelekea kwenye Sifuri 3 hadi ifikapo 2030.

Kwa upande wake Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Mbeya, Dk. Francis Philly alisema hadi sasa Kondom zimeanza kusambazwa mawilayani ambapo tayari Jiji la Mbeya limepokea Kondom laki nane (800,000)na Wilaya ya Mbeya ikiwa imepata Laki saba(700,000).

Naye Afisa usajili vifaa tiba kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Goodluck Gotora alisema Kondom aina ya Zana ni bora kwani zimepitia katika hatua zote muhimu kwa ajili ya matumizi sahihi kwa wananchi.

0 Responses to “ KONDOM YA ZANA RASMI KUZINDULIWA KESHO MKOANI MBEYA ”

Post a Comment

More to Read