Wednesday, August 31, 2016

BABA MZAZI WA DIDA AAGWA RASMI LEO




Leo tarehe 31, Agosti 2016 ndio ilikuwa siku maalumu kwa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Soka nchini, wachezaji pamoja na watu mbalimbali kumuaga marehemu baba mzazi wa golikipa wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na timu ya Young Africans ‘ Yanga’ Deogratus Bonventure Munishi ‘Dida.


Katika kumuaga marehemu mzee Bonventure Munishi walijitokeza watu mbalimbali wakiwemo mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji, makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange Kaburu na wachezaji soka mbalimbali akiwemo golikipa wa zamani wa Timu ya Taifa ambaye pia aliwahi kuichezea klabu ya Yanga Ivo Mapunda.
 




Baba mzazi wa Dida, marehemu Mzee Munishi alifariki tarehe 28 Agosti, 2016 ambapo mazishi ya mzee Munishi yatafanyika Kibosho Mkoani Kilimanjaro.
 



0 Responses to “BABA MZAZI WA DIDA AAGWA RASMI LEO”

Post a Comment

More to Read