Friday, September 2, 2016
JWTZ YALIONYA GAZETI LA TANZANIA DAIMA KWA KUANDIKA TAARIFA YA UPOTOSHAJI
Do you like this story?
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na
gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4290 la tarehe 01 Septemba 2016,
ikihusisha shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika maadhimisho ya miaka 52
ya kuzaliwa kwake na shughuli za kisiasa.
Tunapenda
kuwataarifu wananchi kwamba kazi ya Jeshi ni kulinda na kutetea maslahi ya
Taifa na mipaka ya nchi, aidha, Jeshi letu linafanya kazi kwa kufuata mila,
desturi, nidhamu, kanuni na sheria za Kijeshi kwa weledi wa hali ya juu, hivyo
lisihusishwe na propaganda zozote za kisiasa kwani Jeshi letu ni lenye maadili
ya kitaasisi ya hali ya juu.
Jeshi
ni taasisi ya dola wala si taasisi ya kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na
wanasiasa ni wakati linapotetea na kulinda maslahi ya wananchi. Inaombwa
kuwa makini katika utoaji wa maelezo au malalamiko, iachwe mara moja vyama vya
siasa kuingilia ratiba za Kijeshi.
Ikumbukwe
kwamba tarehe 25 Julai kila mwaka ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa wetu
waliolitumikia Taifa hili kwa umakini na nguvu zote kwa kuleta mafanikio
tunayoyaona, na hii ilipitishwa mwaka 1979 wakati Majeshi yetu yanarudi kutoka
Uganda baada ya ushindi wa vita vya Kagera.
Sherehe
ya mapokezi hayo yalifanyika mji wa Bunazi Wilaya ya Misenye wakati huo Wilaya
ya Bukoba Mkoani Kagera ilipoanzishwa kuwa tarehe hiyo iwe siku ya Mashujaa na
kupitishwa Kisheria, ikabaki siku ya tarehe 01 Septemba kuwa ni siku ya
kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, hivyo jana tulikuwa
tunasherekea siku ya kuzaliwa JWTZ. Ieleweke hivyo na iachwe mara moja
kuchanganya shughuli za Kijeshi na mambo ya Kisiasa, viongozi wa kisiasa wekeni
kumbukumbu zenu vizuri.
Jeshi
linasisitiza wanasiasa ni vizuri wakasoma vema historia ya nchi wanayotaka
kuiongoza na wanayoongoza ili kuepusha upotoshaji, lugha na maneno yanayotolewa
na viongozi wa kisiasa wenye matakwa binafsi kuhusisha shughuli za Jeshi na
siasa zao yanatia ukakasi na kiungulia, awe makini kuongea vitu ambavyo haelewi
na kutokuwa makini zaidi aelewe madhara yanayoweza kutokea kutokana na upotoshaji.
Jeshi
letu linafanya shughuli zake ki weredi.
Imetolewa
na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao
Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P
9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa
Mawasiliano zaidi: 0784-477638
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “JWTZ YALIONYA GAZETI LA TANZANIA DAIMA KWA KUANDIKA TAARIFA YA UPOTOSHAJI”
Post a Comment