Friday, September 2, 2016
MENO YA TEMBO YAKAMATWA KWENYE HIACE IRINGA
Do you like this story?
NA RAYMOND MINJA IRINGA
Jeshi la polisi mkoa wa
Iringa linawashikilia abaria kumi na nne waliokuwa wakisafiri na gari ndogo
aina ya haice iliyokamatwa na meno ya tembo vipande nane vyenye
uzito wa kilogramu 20 vyenye thamani ya sh milioni 66,600.00 walikokuwa
wakisafiri kutoka mbeya kwenda Dar es saalam
Abiria hao wamekutwa
wakiingia mikononi mwa jeshi la polisi baada ya kondakta na dereva wa
gari hilo kuchanja mbuga mara baada ya kugundua polisi wameona nyara hizo
za serekali zinazosakwa usiku na mchana .
Kamanda wa polisi mkoa wa
Iringa Julias Mjengu alisema kuwa tukio hilo lilitokea agust 31 majira ya
saa 18;10 za jioni katika kijiji cha nyololo kata ya nyololo tarafa ya
malangali katika wilaya ya mufindi mkoani Iringa
Mjengi alisema kuwa gari
hilo lilikamatwa na askari no E.7998CPL Kaisi aliekuwa akirudi nyumbani kwake
akiwa katika eneo hilo la mbaramaziwa alisimamisha gari yenye namba za usajili
T377DCX Toyota hiace ikiwa na abiria 14 ndani yake na ilipoikagua aligundua
gari hiyo haina route ya Iringa bali ilikuwa na route ya mbeya
mjini na tunduma
“Baada ya askari kushuku
gari hiyo alimuamuru kundakta kufungua buti la gari ili kuweza kulikagua na
alikutana na mabegi mengi huko kwenye buti lakini katika begi moja jeusi
alipolifungua alikutana na hayo meno ya tembo vipande nane vilivyokatwa
katikati ambapo ni sawa na tembo wawili waliouwawa
Kamanda Mjengi alisema kuwa
mara baada ya askari kuona nyara hizo za serekali dereva wa gari hilo pamoja na
kondakta wake walitimua mbio na kuingia msituni huku wakilitelekeza gari hilo
pamoja na abiria walimukuwa ndani yake.
Hata hivyo alisema
kuwa jeshi hilo linawashikilia wote walimokuwa ndani ya gari hiyo
kwa mahojiano zaidi ili kuweza kubaini ukweli wa tukio hilo huku msako
mkali ukiendelea ili kuweza kuwakamata waliokimbilia porini .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ MENO YA TEMBO YAKAMATWA KWENYE HIACE IRINGA”
Post a Comment