Friday, September 2, 2016
MBUNGE ATAKAN WATU WENYE JINSIA 2 KUTAMBULIKA KENYA
Do you like this story?
![]() |
| Mbunge wa Kenya Issack Mwaura |
Mbunge mmoja nchini Kenya
amelitaka bunge la taifa hilo kupitisha sheria inayotambua jinsia nyengine ya
tatu ili kumaliza ubaguzi dhidi ya wale wanaotumbulika kuwa na jinsia mbili.
Issac Mwaura pia anataka ufadhili wa upasuaji wa kubadili jinsia
pamoja na hamasa ili kukabiliana na unyanyapaa miongoni mwa watu wenye jinsia
mbili.
''Wananiona mimi kama mtu mwenye laana '',mtu mmoja aliyezaliwa
mwanamke na ambaye baadaye alianza kuwa na tabia za kiume aliambia BBC.
Watu wenye jinsia mbili hawatambuliki moja kwa moja kuwa wanaume
ama wanawake.
James Karanja, ambaye anatambulika kuwa mwanamume alisema kuwa
alipozaliwa alikuwa na jinsia zenye utata na wazazi wake walimtambua kimakosa
kuwa msichana.
''Jina langu rasmi ni Waithera,jina nililopatiwa na mamangu baada
ya jinsia yangu kutambulika kimakosa nilipozaliwa''.
''Walidhani mimi ni msichana na kumbe ni mvulana.Ninatoka kutoka
familia ya umasikini kwa hivyo hawakupata fursa ya kunipeleka hospitali kubaini
jinsia yangu''.
Bwana Karanja kwa sasa anafanyiwa upasuaji ,ili kubadilisha jinsia
yake na anasema kuwa matibabu hayo ni ya gharama ya juu sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ MBUNGE ATAKAN WATU WENYE JINSIA 2 KUTAMBULIKA KENYA”
Post a Comment