Friday, September 2, 2016
RAIS MAGUFULI AFIKA KWENYE KABULI LA DKT OMARI JUMA
Do you like this story?
![]() |
| Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli akiomba dua kwenye kaburi la aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma. lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Asubuhi ya
leo tarehe 02 Septemba, 2016 amewasili Kisiwani Pemba ambapo majira ya
Alasiri anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Pemba katika Mkutano wa
hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani hapa.
Mara
baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa Ndege ya Shirika
la Ndege Tanzania (ATCL), Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama
Janeth Magufuli ameelekea katika kijiji cha Wawi Bigilini kilichopo
katika Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba ambako amezulu Kaburi
la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu
Dkt. Omar Ali Juma.
Dkt.
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika
Kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma na wameshiriki Dua ya kumuombea
Marehemu iliyoongozwa na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kiislamu na
Kikristo.
Akizungumza
mara baada Dua, Rais Magufuli amesema anamkumbuka Marehemu Dkt. Omar
Ali Juma kwa ukarimu wake, upendo, kutojikweza, kutobagua watu na
kudumisha amani katika siku zote za maisha yake.Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kudumisha kwa vitendo amani aliyoisimamia Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.
"Mimi
najua huko aliko Marehemu Dkt. Omar Ali Juma anaendelea kuliombea Taifa
hili ili hiyo amani aliyoihubiri katika maisha yake, ili huo upendo
aliousimamia katika maisha yake, ili huo uchapa kazi kwa ajili ya
manufaa ya watanzania wote tuweze kuendeleza kwa mioyo yetu yote" Amesema Rais Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli amewashukuru Wanafamili wa Marehemu Dkt. Omar Ali Juma
kwa uvumilivu na ustahimilivu wao tangu walipoondokewa na mpendwa wao.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pemba
02 Septemba, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)




0 Responses to “ RAIS MAGUFULI AFIKA KWENYE KABULI LA DKT OMARI JUMA”
Post a Comment