Tuesday, September 13, 2016

KILIMANJARO QUEENS WAANZA MASHINDANO KWA KUTOA KICHAPO KIKALI



Timu ya Taifa ya wanawake Kilimanjaro Queens imewashushia kichapo cha goli 3-2 timu ya Rwanda Katika mchezo wao wa kwanza wa mashindano ya Chalenji,  mchezo uliopigwa jana huko Jinja Uganda

Kilimanjaro Queens ndio walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za wapinzani wao mnamo dakika ya 11 ya mchezo kupitia kwa  Asha Rashidi na bao la pili kuwekwa wavuni na Stumai Abdallah katika dakika ya 28

Rwanda walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Ibangarrye Marie ambao mpaka mapumziko  ya mchezo huo goli zilikuwa ni 2-1



Makosa yaliyo fanyika na mabeki wa Kilimanjaro Queens  katika kipindi cha pili yaligharimu timu yao baada ya kujifunga wenyewe kupitia kwa Amina Ally na kufanya Rwanda kupata mabao 2-2

Mnamo dakika ya 65  ya kipindi cha pili  Asha Rashidi alizichungulia tena nyavu za Rwanda na  kuandika goli la 3 Kilimanjaro Queens goli lililowabana mbavu Rwanda na kukubali matokeo hayo
 


0 Responses to “KILIMANJARO QUEENS WAANZA MASHINDANO KWA KUTOA KICHAPO KIKALI”

Post a Comment

More to Read