Monday, September 12, 2016
BWENI PEKEE LA WASICHANA LATEKETEA KWA MOTO
Do you like this story?
Bweni
la Wasichana la Shule ya Sekondari Mwanzi wilayani Manyoni, Mkoa wa Singida,
limeteketea kwa moto na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh50 milioni huku
wanafunzi 42 wakinusurika.
Hilo
ni bweni la shule pekee wilayani Manyoni yenye kidato cha tano na sita.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kukagua bweni hilo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew
Mtigumwe ameagiza timu maalumu iundwe kubaini chanzo cha moto huo.
“Pamoja
na uchunguzi wa awali kuonyesha uwezekano wa moto huo kusababishwa na hitilafu
ya umeme, tusibweteke, lazima uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini chanzo cha
moto huu,” amesema Mtigungwe.
Pia,
amesema kama kuna watu wamehusika, wakamatwe na kufikishwa mbele vyombo vya
sheria.
Mkuu
wa Wilaya ya Manyoni, Geofrey Mwambe amesema mali mbalimbali za wanafunzi zenye
thamani ya zaidi ya Sh25 milioni zimeteketea, huku hasara ya Sh24.3 milioni
ikipatikana kutokana na jengo hilo kuharibika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ BWENI PEKEE LA WASICHANA LATEKETEA KWA MOTO”
Post a Comment