Monday, September 12, 2016

UKAWA WALALA MBELE MECHI YA WABUNGE




Mambo hayajaisha? Ndivyo unavyoweza kujiuliza baada wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia mechi ya mpira wa mguu kati ya timu ya wabunge na Kamati ya Amani ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Wabunge hao wamesusia mchezo huo kwa madai kuwa kuna ajenda ya siri kwenye mchezo huo.

Kutokana na uamuzi huo, badala ya viongozi hao wa dini kucheza na timu ya Bunge, walicheza na timu ya maveterani ya Dodoma, huku taarifa nyingine zikidai kuwa wabunge wamezuiwa kushiriki.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Dodoma, wabunge wa Ukawa wamesema wameacha kwenda kucheza baada ya kutoshirikishwa katika maandalizi ya mechi hiyo.

Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga amesema hawakuenda uwanjani kwa sababu kamati hiyo ilialikwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ambaye wamekuwa na mgogoro naye kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa Timu ya Bunge, Willam Ngeleja alipotafutwa simu yake iliita bila majibu.

Hata hivyo, siku moja kabla ya kuchezwa kwa mechi hiyo Ngeleja alikaririwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akisema mchezo huo ulilenga kuenzi amani kwa Watanzania.
Hata hivyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson amesema wabunge wengi hawakuwepo katika mechi hiyo kwa sababu ni mwisho wa wiki na wengine wameenda mashambani na wengine majimboni.

0 Responses to “UKAWA WALALA MBELE MECHI YA WABUNGE”

Post a Comment

More to Read