Sunday, September 4, 2016
TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYOYA KODI KWA MWEZI AGOSTI
Do you like this story?
Katika
harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa
Wakati, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imejiwekea mikakati mbalimbali ya
kuongeza wigo wa vyanzo vya Mapato pamoja na kukusanya Mapato kikamilifu.
Mikakati
hiyo ni kama ifuatavyo;
Kulifanya
eneo la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu
cha biashara hapa nchini na kuhakikisha kila mfanyabiashara anakuwa na Mashine
ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.
Katika
kutekeleza hilo Mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika jengo
la Al-Falah Towers lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili kurahisisha
upatikanaji wa mashine hizo na kutatua changamoto zinazowakabili
wafanyabiashara katika matumizi ya mashine hizo.
Aidha
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo ametoa
wito kwa wananachi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za
usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo vifuatavyo kwaajili
ya zoezi hilo kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo maana baada ya
tarehe hiyo zoezi hili litahamia mikoa mingine;
Vituo
hivyo vya uhakiki ni pamoja na:
- Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
- Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
- Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
- Wilaya ya Kigamboni – Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja
na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa
kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa
na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji
Wakati
huo huo Bw. Kayombo amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo
la Serikali la kufunga mashine za EFDs kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2016
kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe 1 oktoba na
hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo
hilo.
Katika
kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati
Mamlaka inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la
Thamani -VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla au tarehe 20 ya kila mwezi
badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka hu wa fedha.
Kwa
upande wa walipa kodi zaa makadirio na kodi za makampuni (Corpoaration Tax)
wanakumbushwa kulipa kodi zao mapema mwezi hu wa tisa badala ya kusubiri
msongamano mwisho wa mwezi ambao unaweza kuwasababishia usumbufu
Hivyo
hivyo walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo
wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA
zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.
Kutokana
na mikakti mizuri iliyowekwa na uiongozi wa TRA na serikali Mpaka sasa baadhi
ya mikakati hiyo imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo
ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 TRA imekusanya Trillioni 1.158
ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57. ambapo
Mwezi Agosti Mwaka 2015 TRA ilikusanya Billion 923.
Wito
wetu kwa wanahabari na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kutuunga mkono kwa
kuhimiza kutoa risiti pamoja na kudai risiti katika kila manunuzi pamoja na
kutoa taarifa za dalili za ukwepaji wa kodi wa aina yoyote mahali popote nchini
‘Pamoja
Tunajenga Taifa Letu’
Richard
Kayombo
MKURUGENZI
WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYOYA KODI KWA MWEZI AGOSTI”
Post a Comment