Monday, September 5, 2016
WALIOONGEZA VITI KWENYE BAJAJI WAONDOE MARA MOJA KWANI NI UKIUKWAJI WA SHERIA, MKUU WA MKOA WA MBEYA
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Leo amekutana na waendesha Bajaji kwa lengo
la kusikiliza Kero na kuzitafutia ufumbuzi
Amekubali ombi la waendesha bajaji la kuvunja vyama viwili vinavyovutana na kuundwa Chama kimoja na amemwagiza mkurugenzi kusisimamia uchaguzi huo.
Amekubali ombi la waendesha bajaji la kuvunja vyama viwili vinavyovutana na kuundwa Chama kimoja na amemwagiza mkurugenzi kusisimamia uchaguzi huo.
Ameelekeza watakapopatikana viongozi Mkuu wa wilaya, mkurugenzi jiji, Kamanda polisi barabarani, Sumatra kwa pamoja wakae na uongozi wa bajaji kufanya makubaliano ya njia na vituo kwa lengo la kupunguza msongamano na ajali.
Pia makubaliano yalenge
kulifanya jiji kuwa safi na usalama na watumiaji wengine wa barabara
Kwa walioongeza viti katika bajaji kinyume na utaratibu amewapa mwezi tarehe 30 septemba waoviondoe kwani kwa muundo wa bajaji kuongeza Kiti kwa Dreva ni hatari na ni kinyume cha sheria.
Kwa walioongeza viti katika bajaji kinyume na utaratibu amewapa mwezi tarehe 30 septemba waoviondoe kwani kwa muundo wa bajaji kuongeza Kiti kwa Dreva ni hatari na ni kinyume cha sheria.
Amewapa muda wa kutosha wakubaliane na Kamati na wawajulishe wadau wao ili utekelezaji utakapoanza tarehe moja October hategemei kuona watakakiuka makubaliano
Amewataka jiji kuboresha miundombinu YA barabara ili kuweka mazingira mazuri kwa waendesha bajaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

.gif)

0 Responses to “WALIOONGEZA VITI KWENYE BAJAJI WAONDOE MARA MOJA KWANI NI UKIUKWAJI WA SHERIA, MKUU WA MKOA WA MBEYA”
Post a Comment