Tuesday, September 6, 2016
TAARIFA YA SPIKA JOB NDUGAI KUHUSU RAIS MAGUFULI KUPITISHA MIOSWAADA MITANO.
Do you like this story?
Na
Eleuteri Mangi-Maelezo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia na
kusaini Miswada mitano kutumika kama Sheria kamili za nchi.
Hayo
yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai
mara baada ya kufungua Mkutano wa nne wa Bunge la 11 leo mjini Dodoma.
Miswada
iliyoidhinishwa na Rais ni pamoja Sheria ya Fedha na Matumizi ya mwaka 2016,
Sheria ya Fedha namba 2 ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbambali namba 2 na 4
ya mwaka 2016 na Sheria ya Marekebisho ya Ununuzi ya Umma namba 5 ya mwaka
2016.
Aidha,
Mhe. Spika amewakumbusha Wabunge kusoma na kuelewa kila kinachokuja Bungeni ili
waweze kutekeleza majukumu yao ya kibunge ipasavyo kwa niaba ya wananchi
waliowatuma kufanya kazi hiyo ili kuwaletea maendeleo.
Wabunge
wametakiwa kutekeleza majukumu hayo ya uwakilishi wa wananchi ili waweze
kujadili masuala mbalimbali kwa kuzingatia haki, ustahimilivu, busara, hekima
na kutumia lugha ya staha katika mijadala ya Bunge.
Vile
vile Mhe. Spika amempongeza Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kuongoza vema mkutano
wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19 na kumalizika Juni 30 mwaka huu kwa
kushirikiana na wenyeviti wa Bunge Andrew Chenge, Mussa A. Zungu na Najima
Giga.
Katika
hatua nyingine Mhe. Spika amemshukuru Rais Dkt. Magufuli, Wabunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote walimuombea alipokuwa kwenye
matibabu nje ya nchi pamoja na Madaktari waliomhudumia akiwa kwenye matibabu na
kumshukuru Mungu kwa kumwonesha upendo alipokuwa kwenye mapito ya kuugua.
Katika
mkutano huo wa Bunge yameulizwa maswali 14 ambayo yalielekezwa kwenye Wizara
mbalimbali na kujibiwa kwa llengo la kutolea ufafanuzi masuala yanayotekelezwa
kwa Serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ TAARIFA YA SPIKA JOB NDUGAI KUHUSU RAIS MAGUFULI KUPITISHA MIOSWAADA MITANO.”
Post a Comment