Wednesday, September 7, 2016

ALIYEFANYIWA UPANDIKIZAJI WA KWANZA WA USO AFARIKI


Madaktari nchini Ufaransa wamefichua kwamba mwanamke aliyefanyiwa upasuaji wa kwanza wa upandikizaji wa sura alifariki mapema mwaka huu.
Hospitali moja imesema kuwa Isabelle Dinoire alifariki baada ya matatizo yanayohusishwa na upasuaji huo.

Alifanyiwa upasuaji huo uliochukua saa 15 mwaka 2005 baada ya kujeruhiwa na mbwa.

Madaktari waliutengeza mdomo wake,pua na taya katika upasuaji huo wa kwanza kuwahi kufanyika.

Hospitali hiyo imesema kuwa kifo chake hakikutangazwa hadi sasa ili kulinda faragha ya familia yake



Isabelle si mwanamke wa kwanza kubadilisha sura yake, msanii wa mziki wa Hip Hop nchini Marekani Lil Kim pia alifanya upandikizaji wa sura na kubadili muonekano wake jambo ambalo liliwashangaza mashabiki wengi baada ya kupost muonekano wake mpya katika ukurasa wake wa Instagram.





“Tunamkumbuka” Michael Jackson (Black Amerika) Msanii wa Pop aliepata umaarufu  Mkubwa Duniani pia alifanya upandikizaji wa  pua  na uso wake nakufanya kubadilika kabisa muonekano wake na kuonekana kama mzungu

0 Responses to “ALIYEFANYIWA UPANDIKIZAJI WA KWANZA WA USO AFARIKI”

Post a Comment

More to Read