Monday, September 12, 2016

WATU WATATU WAMEKAMATWA KWA KUIBA NG"OMBE WA RAIS




KAMPALA: Wanaume watatu wanaotuhumiwa kuiba ng’ombe katika shamba binafsi la Rais Yoweri Museveni wa Uganda wamekamatwa. Mmoja kati ya watuhumiwa hao anafanya kazi katika shamba la Rais Museveni, na yeye pamoja na wenzake walikuwa wakiwapeleka ng’ombe hao katika mnada ili kuwauza.

Watuhumiwa hao walikiri kuwa wamekuwa wakiiba ng’ombe kabla ya kukamatwa, alisema Afisa wa Polisi Doreen Kachwo.
Aidha, alieleza kuwa uchunguzi unaendelea na utakapokamilika watuhumiwa wote watapelekwa mahakamani.

Rais Museveni ambaye ameiongoza Uganda kwa miongo mitatu sasa hupenda kutembelea eneo hilo mara kadhaa awapo na wageni kutoka mataifa mbalimbali.


Rais Yoweri Museveni wa Uganda akiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika shamba analofugia ng’ombe.

0 Responses to “WATU WATATU WAMEKAMATWA KWA KUIBA NG"OMBE WA RAIS”

Post a Comment

More to Read