Monday, September 12, 2016
WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA YA WAISLAMU KATIKA SWALA YA IDD EL HAJI
Do you like this story?
Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa, amewataka waumini wa dini
ya Kiislamu kuitumia sikukuu hii ya Idd el Haji kutenda mema na kuungana na
waumini wengine katika kudumisha amani ya nchi yetu.
Waziri
Mkuu akiyasema hayo leo Septemba 12, 2016, kwenye ibada ya sala ya Idd el Haji
iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam
ambapo miongoni mw masheikh maarufu walihudhuria ibada hiyo ni pamoja na Sheikh
Shariff, Sheikh Nurdin Kishki,(mwenyeji wa hadhara), Sheikh Ponda Issa Ponda na
Sheikh Rajab Katimba.
“Kwa niaba ya serikali yenu, nawatakia sikukuu
njema, na ninaomba kuwasilisha salamu za upendo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, pamona na Makamu wa
Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, na niwaombe ndugu zangu muitumie sikukuu hii
kudumisha amani na upendo,” alisema Waziri
Mkuu.
Waziri Mkuu pia alitumia fusa hiyo kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kote
nchini, kuwaombea wananchi wa mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la
ardhi lililosababisha vifo.
Waziri
Mkuu ambaye alihudhuria ibada ya kuaga miili ya watu 16 kwenye uwanja wa
michezo wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera Jumapili Septemba 11, 2016,
alisema kwa sasa kuna majeruhi zaidi ya 100 ambao bado wanapatiwa matibabu.
Tetemeko
hilo lilillopelekea uharibifu mkubwa wa nyumba lilitokea Jumamosi alasiri
Septemba 10, 2016.
Naye
mwenyeji wa Ibada hiyo Sheikh Nurdin Kishki, alimshukuru Waziri Mkuu kwa
kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Temeke, katika swala hiyo
ya Idd.
“Nduhgu zangu napenda nimshukuru Waziri wetu Mkuu kwa kutoka Oysterbay
hadi kufika huku Temeke kuungana nasi katika kutekeleza swala hii ya Idd El
Haji, mwenyezimungu amjalie heri na busara katika uongozi wake,” Alsiema Sheikh
Kishki.
![]() |
| Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam |
![]() |
| Waziri Mkuu, akiteta jambo na sheikh Ponda |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)







0 Responses to “ WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA YA WAISLAMU KATIKA SWALA YA IDD EL HAJI”
Post a Comment