Thursday, November 10, 2016
MAELFU WAANDAMANA MAREKANI KUPINGA USHINDI WA TRUMP
Do you like this story?
Kufuatia
kutangazwa kwa Donald Trump kuwa Rais mteule wa Marekani, wananchi wa Marekani
wameandamana katika miji saba kupinga ushindi huo wa Trump.
Waandamanaji hao wamekusanyika nje ya mnara maarufu wa Trump ‘ Trump Tower’ mjini New York wakipaza sauti za kumpinga Trump. Wengine walionekana nje ya Ikulu ya Marekani wakipaza sauti kuwa “Not my president” (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.
Wengi
wa waandamanaji walioongea na CNN wameelezea kuwa wana wasiwasi sana kuhusu Trump
kwavile kuongoza Marekani sio kama kuiongoza nchi yoyote duniani.
“Kwa
matokeo haya tumeiangusha Dunia. Trump hakustahili kuwa Rais. Nahisi watu
walipiga kura kwa hasira lakini Trump ni hatari kwa dunia,” alisema mmoja wa
waandamanaji aliyejitambulisha kwa jina la James Betwell kutoka Califonia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAELFU WAANDAMANA MAREKANI KUPINGA USHINDI WA TRUMP”
Post a Comment