Thursday, November 10, 2016
TRUMP AWASILI WHITE HOUSE
Do you like this story?
Rais mteule wa Marekani Donald
Trump amewasili katika Ikulu ya White House, kwa mujibu wa maafisa nchini
Marekani.
Hata hivyo aliingia akitumia mlango tofauti na kuwasili kwake
hakukunaswana kamera za waandishi wa habari.
Anatarajiwa kuwa kwenye mazungumzo na Rais Obama wakati huu.
Licha ya tofauti zao, bwana Obama siku ya Jumatano alikishauri
kikosi chake kufanya jitihada zaidi kuhakisha kuwa kuna mafanikio kwenye
shughuli ya kupokeza madaraka kwa Republican mwezi Januari.
Mapema kikosi cha kampeni ya Trump kilikutana na washauri kujadili
masuala kuhusu siku za kwanza 100 za Trump kama rais na uteuzi muhimu katika
nyadhifa za serikali.
Majina yaliyotajwa ni kati ya wale waliomuunga mkono Trump kutoka
mwanzo akiwemo aliyekuwa spika Newt Gingrich, maseneta Jeff Sessions na Bob
Corker pamoja na aliyekuwa meya wa New York Rudy Giuliani.
![]() |
Waandishi wa habari wakimsubiri Trump White House |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRUMP AWASILI WHITE HOUSE”
Post a Comment