Thursday, December 15, 2016
BABA ACHINJA WANAWE WAWILI NA KISHA KUJINYONGA
Do you like this story?
Watoto
wawili wenye umri wa miaka mitatu na sita wa Kijiji cha Patane Kata ya
Mambamiamba wilayani Same, wameuawa kwa kuchinjwa na panga na baba yao
mzazi Yohana Greson (26) na yeye mwenyewe kujining’iniza kwenye paa la nyumba.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,
Wilbroad Mutafungwa, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 13, mwaka huu
majira ya saa tano asubuhi katika Kijiji cha Patane.
Kamanda
alisema baba huyo alifanya tukio hilo la kutisha baada ya mkewe Eva Tumaini
(29) mkazi Kijiji cha Ghona kwenda shambani na kumwacha mumewe nyumbani akiwa
na watoto wawili, Esta Yohana na Tumaini Yohana, ambapo alichukua panga na
kuwachinja na yeye kujinyonga kwa kamba.
Alisema
Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba uchunguzi wa awali
umebaini marehemu huyo alikuwa na tatizo la kifafa.
Alisema
miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same kwa
ajili ya uchunguzi zaidi na kwamba marehemu hakuacha ujumbe wowote na uchunguzi
ukikamilika ndugu za marehemu watakabidhiwa miili hiyo kwa ajili mazishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BABA ACHINJA WANAWE WAWILI NA KISHA KUJINYONGA”
Post a Comment