Saturday, December 17, 2016
HAYA NDIO MASHARTI YA DURU LA PILI LIGI KUU TANZANIA BARA
Do you like this story?
Duru la Pili
la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza leo Jumamosi Desemba 17
kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kufanyika siku ya Jumapili
Desemba 18, mwaka huu.
Katika mechi za kesho, Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young
Africans SC ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo
utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Licha ya kwamba mwenyeji wa mchezo huo ni JKT Ruvu ambayo uwanja
wake wa nyumbani mara nyingi huwa ni Mabatini ulioko Mlandizi, lakini kwa
mujibu wa Kanuni ya 6 (5) na (6) ya Ligi Kuu Bara, mechi zake za nyumbani dhidi
ya Simba, Young Africans na Azam FC, hufanyika Uwanja wa Uhuru.
Michezo mingine ya leo ni Kagera Sugar kuwa mgeni wa Mbeya City
kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting ya Pwani itakuwa
mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ilihali
Mwadui ya Shinyanga itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa
Mwadui Complex.
Jumapili, Desemba 18, mwaka huu Mbao FC ya Mwanza itacheza na
Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Ndanda
itakuwa mwenyeji wa Vinara wa Msimamo katika Ligi Kuu ya Vodacom, Simba kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
African Lyon ya Dar es Salaam itaikaribisha Azam FC pia ya Dar es
Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru jijijini siku hiyo ya Jumapili wakati Majimaji ya
Songea itakuwa Mbeya kucheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, limetoa masharti kadhaa
likitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom kufuata.
Masharti hayo, ni kwa klabu kutumia makocha wenye sifa kwa mujibu
wa kanuni ya 72 ya Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Kuu ya
Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) na kwa mujibu wa kanuni hiyo, makocha
wanaopaswa kukaa kwenye benchi la Ligi kuu kwa msimu huu wasipungue sifa ya
kuwa na leseni B ya CAF.
Pia kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza na Pili, masharti ni lazima
makocha wawe na sifa za kuzinoa timu hizo ambazo zimeanishwa kwenye kanuni za
ligi husika.
Kadhalika, tunaagiza klabu kutotumia wachezaji wa kigeni au
makocha kama hawana vibali vya ukaazi na kufanya kazi kutoka Idara ya Uhamiaji
nchini iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ HAYA NDIO MASHARTI YA DURU LA PILI LIGI KUU TANZANIA BARA”
Post a Comment