Wednesday, December 21, 2016
MKUU WA MKOA AHAIDI KULIFANYA SOKO LA NDIZI KIWIRA KUWA SOKO LA MATAIFA.
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Makalla akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe(kushoto) na Diwani wa Kata ya Kiwira wakielekea kuangalia Soko ambalo litakuwa la kimataifa. |
Mwonekano wa Soko la Wafanyabiashara katika Wilaya ya Rungwe kiwira. |
Wakina mama wakiwa kwenye Biashara zao za kila siku za Kuuza ndizi kiwira |
MKUU wa Mkoa Wa Mbeya Amos Makalla leo ametembelea soko la ndizi la Kiwira na kufanya mkutano wa hadhara na kueleza Azma ya serikali ya Mkoa wa Mbwya kuliboresha soko la ndizi la kiwira kuwa soko la kimataifa kwani mpska SASA ni wafanyabiashara wengi toka nchi za jirani wanalitumia soko hilo
Kuboresha kwa soko Hilo kutaongeza biashara na litarasimisha biashara na kuongeza mapato kwa wafanyabiadhara na serikali.
Aidha amekabidhi Fedha taslimu shilingi milioni Mbili ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwezi uliopita kwenye harambee ya kuchangia mradi wa Maji Kijiji cha Ilundo kata ya Kiwira.
Amekemea tabia ya baadhi ya wanasiasa kuendekeza malumbano ya kisiasa na kukwamisha shughuli za maendeleo na amewataka kwa pamoja washirikiane kukabiliana na changamoto yaujenzi wa vyoo na madarasa katika Shule za msingi na sekondari.
Amesema maendeleo yasichanganywe na itikadi ya vyama vya Siasa sasa hivi wananchi washiriki shughuli za maendeleo na Siasa ni mwaka 2019 kwenye uchaguzi wa serikali za vitongoji,Vijiji na mitaa na uchaguzi Mkuu 2020
Hivyo kwa sasa kama kiongozi wa Kijiji, Diwani au mbunge wananchi wampe ushirikiano bila kujali katoka Chama Gani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKUU WA MKOA AHAIDI KULIFANYA SOKO LA NDIZI KIWIRA KUWA SOKO LA MATAIFA.”
Post a Comment