Friday, December 16, 2016

KAMA HUNA CHOO JIANDAE SERIKALI IMETANGAZA KIAMA KWAKO




Serikali imesema ifikapo juni tano mwakani itaendesha operesheni nchi nzima ya kuwakamata na kuwapeleka katika vyombo vya sheria kaya ambazo zitabainika kuwa zimeshindwa kuwa na vyoo bora kutokana na utafiti kubaini kaya ambazo zina vyoo bora nchini ni chini ya asilimia 20.

Kwa mujibu wa waziri wa afya, maendeleo ya jamii. jinsia, wazee na watoto hali hiyo inatokana na takwimu kubaini kuwa ni 19 tu ya wakazi wa mijini wana vyoo bora huku asilimia kumi tu ya wakazi wa vijijini wakitumia vyoo bora na tayari muda wa miezi sita uliotolewa na serikali kwa kaya zote kuwa na vyoo hivyo unazidi kwenda.

Waziri Ummy Mwalimu ameweka msisitizo huo wakati akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria na kusema kuwa kamwe hawezi kuvumilia watanzania wakiendelea kuumwa magonjwa yanayozuilika yakiwemo yale yanayosababishwa na ukosefu wa vyoo bora.

Naye mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Taifa ya takwimu Dr. Albina Chuwa amesema wamefanya utafiti huo ili kuweza kuyabaini yanayojiri katika sekta ya afya na kuiwezesha serikali kubaini madhaifu yaliyopo sambamba na kubuni mikakati ya kutatua changamoto hizo.

0 Responses to “ KAMA HUNA CHOO JIANDAE SERIKALI IMETANGAZA KIAMA KWAKO”

Post a Comment

More to Read