Friday, December 16, 2016

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU SIASA MASHULENI




Serikali imepiga marufuku siasa kuingilia utekelezaji wa majukumu ya kitaaluma kwenye sekta ya elimu na kuwaagiza wakurugenzi na makatibu tawala wa halmashauri miji na majiji kuwalinda na kuwasaidia walimu wakuu na wakuu wa shule watakaoripoti kubugudhiwa na wanasiasa kwa namna yeyote ile.

Agizo hilo linatolewa na wizara ya elimu sayansi teknolijia na mafunzo ya ufundi Profesa Joyce Ndalichako katika mkutano na wajumbe wa shirikisho la wakuu wa shule za sekondari nchini TAHOSSA ambao awali walimueleza Mhe waziri kuwa hivi sasa wanashindwa kutekeleza majukumu yao ipasvyo kutokana na kuhofia wanasiasa ambao wamefikia hatua hata ya kuwaadhibu.

Mbali na changamoto hiyo ya wanasiasa wakuu hao washule pia wakabainisha matatizo lukuki wanayokumbana nayo ikiwemo mazingira mabovu ya kazi ukosefu wa walimu, vifaa vya kujifunza na kufundishia huku wakiiomba serikali kuruhusu ajira kwa walimu kwani kuna uhaba mkubwa hasa maeneo ya vijijini.

Nao wadau wa elimu walioshiriki kwenye mkutano huo wamesema imefika wakati sasa elimu inayotolewa nchini kuwaandaa wanafunzi wanaohitimi elimu katika ngazi mbalimbali kuondokana na fikra za kuajiriwa badala yake wajiajiri kwani nchi nyingi zilizopiga hatua walitumia mfumo huo.

Katika mkutano huo pia wakuu hao wa shule wakatoa tuzo kwa wadau mbalimbali ambao mchango wao umetambulika katika kusaidia elimu kusonga mbele.

0 Responses to “SERIKALI YAPIGA MARUFUKU SIASA MASHULENI”

Post a Comment

More to Read