Friday, December 16, 2016
MIMBA ZA UTOTONI ZASHIKA KASI MKOA WA IRINGA
Do you like this story?
na
fredy mgunda,Iringa
Shirika
lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) limeendelea kukemea na kutoa
elimu juu ya ndoa za utotoni kwa kuwa zinarudisha maendeleo nyuma ya wasichana
wa jamii ya kimasai.
Akizungumza
na blog hii Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program
(IOP) Edson Msigwa alisema kuwa tatizo la ndoa za utotoni katika kabila la
wamasai bado ni kubwa.
Msigwa
alieleza jinsi gani wanavyofanya shughuli za kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa
za utotoni katika jamii ya wamasai
“Tunajitahidi
kuwafikia jamii zote za wilaya ya kilolo mkoani iringa kwa lengo la kutoa elimu
lakini tunakumbana na changamoto kutoka kwa wazazi ambao bado wana mila potofu
hasa huku umasaini”alisema Msigwa
Aidha
Msigwa alisema kuwa kila siku ndoa za utotoni zinaongezeka huko vijijini
na kuitaka serikali kukubali takwimu wanazozitoa kwa kuwa zinaukweli.
“Sisi
hapa Ilula Ophan program (IOP) tunaishi na wasichana wa kabila la kimasai
wafanikiwa kukimbia kuozeshwa wakiwa na umri mdogo hebu mwangalie huyo motto
joyce alivyo alitakiwa aolewe na umri huu wa miaka kumi nan ne je unafikiri ni
haki jamiii inatakiwa kubadili na serikali inatakiwa kuongeza juhudi kulitatua
hili”alisema Msigwa
Naye
mmoja wa wasichana wa kimasai aliyekimbia kuolewa akiwa na umri mdogo Joyce
Hassani alisema kuwa msichana wa kimasai wakimaliza elimu ya msingi
wanalazimishwa kuolewa na familia yake.
“Mimi
na mwenzangu tumemaliza shule tu wametupeleka kucheza ngoma kisha kutaka
kutuozesha lakini mungu mwema tulifanikiwa kukimbia na kufika hapa Ilula Ophan
program (IOP) japo kuwa wanaume wa kimasi wanakuja hapa kituoni mara kwa mara
kutaka kutuiba turudi kule umasaini ili tukaolewe hasa kaka zangu”alisema joyce
Joyce
ameiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kupambana na mila
potofu zinazowapotezea malengo wasichana wa kimasai.
“Angalia
tunavyoteseka saizi tunaishi kama watoto yatima wakati wazazi wetu wapo na wana
afya zuri kabisa lakini tatizo kubwa sisi wasichana wadogo wa kimasai tunaolewa
tukiwa na umri mdogo sana tunaomba jamii iamuke na kutusaidia kutatua tatizo
hilo.”alisema Joyce
Zipo
sababu nyingi na ushahidi mwingi wa kisayansi, unaonyesha kuwa, ndoa na mimba
katika umri mdogo ni hatari kwa afya na mstakabali wa maisha yake na mtoto
wake.
Wasichana
wanaopata ujauzito na kujifungua katika umri mdogo wengi wao pia hupata tatizo
la fisitula - Vescovaginal fistula.
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na chama cha waandishi wahabari wanawake (TAMWA)
umeonesha kuwa katika mwaka 2012-2013 matukio 228 ya mimba na matukio 42 ya
ndoa za utotoni yaliripotiwa nchini tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MIMBA ZA UTOTONI ZASHIKA KASI MKOA WA IRINGA”
Post a Comment