Friday, December 16, 2016
WANAWAKE MBEYA WAONGOZA KWA KUWATANDIKA WANAUME
Do you like this story?
Na
ROSE CHAPEWA, MBEYA
WANAUME
111 mkoani Mbeya wameripoti kufanyiwa ukatili wa kimwili, huku wengine 14
wakidaiwa kufanyiwa ukatili wa kingono na wenza wao.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Yahya Msuya alisema hayo wakati
wa Kilele cha Maadhimisho ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Alisema
katika matukio 2,890 waliyopokea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Mbeya , kwa kipindi cha mwaka mmoja, hali ilikuwa tofauti na
ilivyozoeleka.
Alisema,
hivi sasa wanaume wamekuwa na mwamko wa kutoa taarifa za kufanyiwa
ukatili wa kimwili na kingono na wanawake, lakini ukatili wa kipigo unachukua
nafasi kubwa.
“Watu
wengi wamezoea kuwa wanaofanyiwa ukatili ni wanawake tu, sasa hivi hali imekuwa
tofauti kati ya matukio 451 ambayo tumeyapokea katika hospitali yetu, matukio
111 ni ya wanaume kufanyiwa ukatili wa kimwili.
“Hivyo
utaona kuwa sasa hivi elimu tunayoitoa watu wameanza kuelewa na aibu
imeanza kutoweka ,sasa wanaume wanaleta taarifa,” alisema Dk. Msuya.
Alisema
kutoka na matukio hayo, matukio 1491yalikuwa ni ukatili kwa watoto na kwamba
wote waliofanyiwa ukatili wa kijinsia, baada ya kuwafanyia
uchukunguzi wa kidaktari baadhi walibainika kuwa na maambukizi ya VVU.
Kwa
upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari,
alisema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2015 walipokea
matukio ya unyanyasi wa kijinsia wa kingono 1281na kuanzia Januari hadi Juni
mwaka huu walipokea matukio ya aina hiyo 661.
“
Katika haya matukio ambayo yameripotiwa hapa kwetu , matukio ya ukatili wa
kingono yameonekana kuchukua nafasi kubwa sana, lakini tunashukuru yanazidi
kuripotiwa , inaonesha kuwa sasa hivi jamii imekuwa na mwamko mkubwa sana
wa kutoa taarifa, na kufahamu yale wanayofanyiwa” Alisema Kidavashari.
Aliwaomba
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na taarifa za siri
pale wanapoona wanafanyiwa vitendo vya kikatili ili kusaidi wahusika kukamatwa
na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Naye
Afisa wa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya Haika Temu alisema katika kipindi cha
mwaka wa fedha uliopita wa 2015/16 ,ofisi yake ilipokea matukio 400, ambayo
yalihusiana na masuala ya utelekezwaji wa familia.
Alisema
akina mama wengi walikuwa wakilalamikia wenza wao kuwaachia watoto bila msaada
wowote wa matunzo na wengine kutelekezwa bila kujua wenza wao walipo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WANAWAKE MBEYA WAONGOZA KWA KUWATANDIKA WANAUME”
Post a Comment